Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy: Nimejipa likizo kumuomboleza Ruge Mutahaba

Sat, 23 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Msiba wa Ruge Mutahaba huenda umeisha kwa watu wengine, lakini kwa baadhi akiwamo mwanamuziki Nandy bado ngoma mbichi.

Mwanamuziki huyo aliyejitambulisha kuwa rafiki wa karibu wa Mutahaba anaendelea kuomboleza na itamchukua mwezi mmoja zaidi kuanzia sasa.

Ikiwa imepita takribani mwezi mmoja tangu Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji huyo wa Clouds Media Group, afariki dunia, mwanamuziki Nandy ameamua kujipa muda wa kupumzika kama njia moja ya kumuomboleza.

Ruge alifariki Februari 26, mwaka huu akiwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu, msiba ambao uliwagusa Watanzania wengi kutokana na mchango aliotoa kwa watu mbalimbali enzi za uhai wake.

Akizungumza na Mwananchi, Nandy ambaye ambaye jina lake halisi ni Faustina Charles, alisema msiba huo umemfanya apumzike ikiwemo kutofanya mahojiano yoyote na vyombo vya habari kuhusiana na kazi zake. Kama vile haitoshi alisema hata baadhi ya shoo amezitolea nje na ataanza kurudi tena ifikapo Mei mwaka huu.

“Nisingependa kuongea lolote kwa sasa kwani nimeamua kujipa muda wa kupumzika na nitarudi tena Mei kwani kuna hata shoo nimepata lakini nimezikataa,” alisema .

Wakati wa msiba, Nandy aliibua gumzo baada ya kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza namna alivyosikitishwa na kifo hicho cha Ruge hali iliyotafsiriwa kuwa alikuwa na ukaribu wa zaidi ya muziki na Mkurugenzi huyo.

Ujumbe huo ulizua gumzo zaidi pale Nandy alipoambatanisha na video iliyokuwa ikimuonyesha Ruge akiwa nyumbani kwake usiku akicheza na mbwa, mbwa ambaye pia siku za nyuma alionekana akicheza naye.

Kama vile haitoshi wakati wa shughuli ya kuaga, zilizofanyika ukumbi wa Karijee Jijini Dar es Salaam, Nandy alionekana kukaa wakati wote eneo la wanafamilia jambo lililozua maswali zaidi na hata baada ya kumaliza kuzika kijijini kwao Kiziru, Mkoani Bukoba alionekana katika picha mbalimbali na wanafamilia wa Ruge.

Nandy ni kati ya wasanii ambao wamepikwa katika Nyumba ya Kukuza Vipaji (THT), ambayo pia alikuwa akiisimamia Rugen a tangu kuingia huko ameshaachia vibao mbalimbali ikiwemo ‘Nagusagusa’, ‘Kivuruge’, ‘Ninogeshe’ ‘Aibu’ na Hazipo aliyoiachia mwezi mmoja uliopita.



Chanzo: mwananchi.co.tz