Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy: Mimi na Zuchu ni marafiki

Zuchu Nandy M.jpeg Nandy na Zuchu

Sat, 6 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Nandy amekanusha kuhusu taarifa kwa alimtumia mtangazaji Mwijaku kimlipa pesa ili amchafue msanii mwenzake, Zuchu kwa kile kilichodaiwa kwamba ni ugomvi wa kibiashara.

Akizungumzia sakata hilo ikiwa ni wiki chache baada ya mazungumzo yake na Mwijaku kuvuja, Nandy amesema ana maelewano mazuri na ni marafiki na Zuchu wala hajawahi kumchafua.

"Mimi sikupanga chochote kumchafua Zuchu ama msanii mwenzangu yeyote, ni mambo tu ya mitandaoni hata yeye anajua. Nimepitia mambo mengi na nyie mnaona mitandaoni, ila mimi huwa sio mtu wa kutoka mitandaoni na kuanza ku-battle, huwa nanyamaza tu.

"Zuchu ni rafiki yangu, tunachati sana, tunashauriana mambo mengi. Mtu mwingine anaweza kudhani sisi ni maadui hapana, sisi ni wasanii, sisi ni marafiki sana. Mambo ya kupambanaishwa yapo tu, nimepambanishwa na akina Rubby na wasanii wengine wengi, lakini mimi naenda kwenye njia yangu sifuati watu wanasema nini.

Nandy ameongeza kuwa mara ya mwisho kuchati na Nandy ni baada ya Harusi na kwamba Zuchu alimpongeza baada ya kufunga ndoa na Billnass.

Kuhusu kudaiwa na Mwijaku, Nandy amesema hadaiwi hivyo Mwijaku aendelee kupiga kelele mitandaoni akimaliza kama atakuwa na nia watazungumza kuyamaliza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live