Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy: Mimba siyo ugonjwa

Nandy Billnass Nandy na Billanass

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Faustina Charles almaarufu Nandy The African Princess; ni malkia wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye amezidisha ripoti za ujauzito kwa mara nyingine tena baada ya kutoka na vazi lililowaacha baadhi ya mashabiki wake na maswali.

Kurasa kadhaa za udaku zilimfikia mwimbaji huyo kwa ujumbe wa pongezi, jambo ambalo lilimlazimu kujibu.

Katika moja ya jumbe hizo, Nandy alijibu kwa kejeli maswali ya kama ana mimba au la bila kukanusha au kukubali.

“Umegundua nini kwenye picha hii," mmoja wa mashabiki wake aliuliza. Kwa haraka, Nandy alijibu ujumbe wa shabiki huyo na kusema; “Kwamba huyo dada ana mimba anaifichaaaa yaaani hata sijui kwa nini anafanya hivyooo khaaaa...”

Shabiki mwingine alifika kwa mwimbaji huyo akimwambia kuwa mimba siyo ugonjwa; “Nandy mimba siyo ugonjwa…” Naye Nandy akajibu; “Kwani nimesema naumwa…”

Hii si mara ya kwanza kwa Nandy kulazimishwa kujibu tetesi za ujauzito. Januari, mwaka huu, Nandy alikanusha tena madai kwamba alikuwa na ujauzito wa mchumba wake Billnass.

Nandy aliweka wazi kuwa, hakuwa na ujauzito na kuongeza kuwa atakapopata ujauzito habari hizo hazitafichwa kwa mashabiki wake kwani hazifichiki.

Wakati hayo yakiendelea, jana Jumapili lilikuwa ni tangazo la pili kanisani la Nandy na Billnass kutarajia kufunga ndoa Julai 16, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live