Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy: Kumzuia Linah kuwa karibu na Billnass ni ushamba

Linah Na Billnass Na Nandy Nandy: Kumzuia Linah kuwa karibu na Billnass ni ushamba

Fri, 5 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ amesema haoni tatizo kwa mumewe, Billnass kupiga picha ama kuwa karibu na Linah ambaye anasemekana alishawahi kuwa ex wake miaka ya nyuma.

Nandy amesema Nenga na Linah wote ni wasanii kwa hiyo suala la kupiga picha pamoja ni kawaida wala watu hawapaswi kuwanenea mabaya wala yeye hahisi jambo baya dhidi yao.

“Kuona picha ya Linah na Billnass sijawaza kitu chochote kiubaya, sababu sisi hatuwezi kukaa na kuulizana mambo ya ma-ex. Watu wanajua mimi na Nenga tupo kwenye uhusiano tangu mwaka 2016, kwa hiyo hata kama alikuwa ni ex ina maana ni nyuma sana.

“Linah ni rafiki yangu, pia ni rafiki wa Billnass, wana-vibe, sio kitu kibaya. Nilishasikia kama walikuwa kwenye mahusiano huko nyuma lakini siwezi kuuliza, nitauliza kama atakuwa kwenye mahusiano na mtu wakati tayari nilikuwa nimeshaingia naye kwenye mahusiano, lakini ya huko nyuma hakijawahi kutokea kwenye maisha yangu.

“Billnass hajawahi kuwa karibu na mtu yeyote ambaye nimeambiwa alishawahi kuwa naye kwenye uhusiano, picha na Linah pale tulikuwa kwenye shoo na tunapiga picha pamoja, sasa kwa nini asipige naye picha, kwa sababu tu ni ex wake? Hapana.

“Linah na Billnass wote ni wasanii, mimi na Billnass kwa sasa ni mke na mume, tushavuka huko, kwa hiyo huwezi kusema we Linah unajua ushawahi kuwa ex? Usimsogelee mume wangu, huo ni ushamba. Linah na Nenga wanakaa wanapiga stori, yani fresh tu. Mimi na Linah ni marafiki, tunachati sana na tuna mipango yetu ya Mwanza mingi tu,” amesema Nandy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live