Menu ›
Burudani
Tue, 16 Aug 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Faustina Charles Mfinanga almaarufu Nandy au Nandera; ni malkia wa muziki nchini Tanzania ambaye anasema kuwa, hana ugomvi na msanii yeyote na kwamba anaongea na wote na anawapenda.
Nandy ambaye ni mke halali wa rapa Billnass anasema kuwa, watu wengi wanadhani kwamba hana ushirikiano na wasanii wengine, lakini hawajui tu kilichopo ndani yake.
“Mimi nipo vizuri sana na wasaniii wenzangu, sina ugomvi na msanii yeyote, ila wengi wa mashabiki wetu wanapenda kuweka chuki kwa wasanii,” anasema Nandy ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Bye akiwa na Billnass au Nenga.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live