Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Nandy Festival’ ya Tanga wanawake pekee kushambulia jukwaa

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanamuziki nchini Tanzania, Faustina Mfinanga maarufu Nandy, katika tamasha lake la ‘Nandy Festival’ litakalofanyika mkoani Tanga ameamua kuchukua wasanii wa kike pekee.

Tayari wasanii mbalimbali wameshasainiwa kushiriki kwenye tamasha hilo litakalofanyika Agosti 3, 2019 akiwemo Mwasiti, Gigy Money, Amber Lulu, Isha Ramadhani, Linah na Rosa Ree huku akiahidi kuongeza wengine.

Akizungumza jana Julai 26, 2019  na Mwananchi, Nandy alisema huo ni ubunifu walioamua kuja nao na menejimenti yake kama njia ya kuonyesha wanawake wanaweza kufanya shoo wenyewe bila uwepo wa wanawake.

“Katika kulifanikisha hilo hata DJ atakuwa mwanamke ambaye ni DJ Mumy, ” alisema Nandy anayetesa na wimbo wa ‘Halleluya’ alioshirikishwa na msanii Willy Paul kutoka nchini Kenya.

Kama vile haitoshi alisema anajisikia vizuri kufanya hivyo, ukizingatia hajawahi kuona shoo ya wanawake tu huku akieleza anaamini wanawake wanaweza.

Hili ni tamasha la tatu kufanyika, likiwa limetanguliwa ni lile lililofanyika Bukoba mkoani Kagera na lile la Sumbawanga Mkoa wa Rukwa.

Pia Soma

Tamasha la Tanga  linatarajiwa kufanyika viwanja vya Mkwakwani huku kiingilio kikiwa Sh5000.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz