Jony Ive ni mbunifu mashuhuri kutoka Uingereza na alikuwa Afisa Mkuu wa Ubunifu kwenye kampuni ya Apple.
Anajulikana sana kwa kazi yake ya ubunifu katika bidhaa maarufu za Apple kama vile iMac, iPod, iPhone, na iPad.
Ushirikiano wake na Steve Jobs, mwanzilishi mwenza wa Apple, unatambulika sana kwa mapinduzi yake katika sekta ya teknolojia na ubunifu.
Jony Ive aliongelea kuhusu kile kitu Steve Jobs alimfundisha kuhusu kuwa focused:
"Hii inaongelewa sana na ni rahisi lakini bado inanishangaza jinsi watu wachache wanazingatia hili. Steve alikuwa mtu mwenye umakinifu wa ajabu zaidi niliyekutana naye maishani mwangu.
Umakinifu si kitu unachotamani. Huamui kwamba Jumatatu 'Nitakuwa makini.' Ni kujiuliza kila dakika Kwa nini bado tunazungumzia hili? Hiki ndicho tunachofanyia kazi.
Moja ya vitu ambavyo Steve angeniambia [binafsi] kwa sababu alikuwa na wasiwasi sikuwa makini angeuliza umesema hapana kwa vitu vingapi?
Ningemwambia nimesema hapana kwa hiki na nimesema hapana kwa kile. Lakini alijua sikuwa na nia ya kufanya vitu hivyo. Hakukuwa na kujinyima kwa kusema hapana.
Kuwa makini/focused inamaanisha kusema hapana kwa kitu ambacho kila mfupa mwilini mwako unafikiri ni wazo la ajabu, unaamka ukilifikiria, lakini unasema hapana kwa sababu unafocus na kitu kingine."
Unaweza kufikia mengi unapokuwa makini.