Msanii mkongwe wa Muziki nchini Kenya, Nameless ambaye ni baba wa mabinti watatu amefichua kwamba hawezi kuzaa mtoto mwingine tena, akisema ameshafanya mchakato wa upangaji uzazi kwa wanaume, Vasektomia.
Akizungumza na mwanablogu Vincent Mboya katika uzinduzi wa mradi wa Talanta Hela katika ikulu ya Nairobi, Nameless alisema kuwa hana mpango wa kupata mtoto mwingine tena na hivyo aliamua kuchukua majukumu ya kupanga uzazi.
“Tushafunga, nimeenda vasektomia. Niliona nichukue majukumu mikononi mwangu. Tumefunga. Kwa wakati huu niliona watoto watatu wa kike wako sawa na tunahisi kubarikiwa sawa, Shiru (binti kitinda mimba) anatuweka bize,” alisema @namelesskenya ambaye ni mume wa msanii @wahukagwi wakiwa kwenye ndoa kwa miaka 18 sasa.