Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nameless ampiku mkewe kupenda viatu

8863 Name+pic TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuna usemi kuwa rafiki wa kweli wa mwanamke ni viatu. Hii imetokana na ukweli kwamba wanawake hununua viatu mara nyingi zaidi kuliko wanaume kwa kuwa hupenda kulinganisha rangi, mavazi na mapambo ya mwili. Kwa wanandoa mastaa Wahu na Nameless ni tofauti kwani mwanamume katika familia hii ndiye anayeongoza kwa kununua viatu mara nyingi zaidi kuliko mkewe.

Wahu ametoboa kuwa mumewe hutumia fedha nyingi kununua viatu na mara nyingi zaidi kuliko yeye.

Anasema kwa kawaida anapotaka kununua viatu huzunguka madukani kuchagua lengo ikiwa ni kulinganisha bei kabla ya kuamua kipi cha kununua.

Kwa Nameless ni tofauti kwani hununua kila kiatu kinachomvutia bila kujali gharama au rangi kitu ambacho Wahu anasema kinamkera.

“Yaani mume wangu anatumia hela nyingi kwenye viatu na mbaya zaidi haangalii rangi, hivi mtu unawezaje kuwa na pea nane za viatu vya rangi moja, yaani hata ukibadilisha watu hawajui?” anahoji Wahu.

Chanzo: mwananchi.co.tz