Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Najutia kuvaa top, Mzungu alinidanganya akaniacha - Hamisi BSS

Hamisi Mks Najutia kuvaa top, Mzungu alinidanganya akaniacha - Hamisi BSS

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, maarufu kama Hamisi BSS amesema kuwa anajuta kumsikiliza aliyekuwa mpenzi wake kwa kuvaa nguo za kike ili ampende lakini mwisho wake akaambulia kuachwa.

Hamisi miezi michache iliyopita ali-trend kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana amevalia 'top' jambo ambalo liliibua maswali mengi na yeye kujibu kuwa mpenzi wake huyo ndiye alimshawishi kuvaa vile.

"Sasa hivi siko na mzungu tena, ni miezi nane sasa tangu tulipoachana amerudi nyumbani kwao alisema muda wa kuishi Tanzania umeisha. Watu wengi wanadhani ukiwa kwenye mahusiano na mzungu basi umeyapatia maisha, sio kweli, mimi pesa kubwa ambayo nimewahi kupewa na mzungu ilikuwa ni elfu 50"

"Ameondoka lakini moja ya kitu ambacho alinitaka nikifanye na najutia mpaka leo ni kupiga picha na kitop, kwa wakati ule nilikuwa naona ni sahihi lakini kwa sasa najutia sana.

"Tulikuwa tunaishi wote yeye ndiye alikuwa ananilipia kodi, kodi ilikuwa ni zaidi ya elfu 50 lakini baada ya kurudi kwao ilinibidi nije kupanga uswahilini chumba cha elfu 30 maana sina uwezo wa kupata elfu 50 kwa mwezi.

"Maisha yangu ni magumu kiasi, sina kitanda nalala chini kwenye godoro, natumia jiko la mkaa sina uwezo wa kununua gas, sina kabati la kuwekea nguo naweka kwenye kamba.

"Kwa mwingine ni maisha magumu lakini kwangu kuna unafuu kwasababu leo yangu ina unafuu kuliko jana, Alhamdulillah, siwezi kuigiza maisha, haya ndiyo maisha yangu," amesema Hamiss BSS alipotembelewa nyumbani kwake na Zamaradi TV

Chanzo: www.tanzaniaweb.live