Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naira wa Jua Kali apigwa hadi mimba yachoropoka

Naira Jua KALI Naira wa Jua Kali apigwa hadi mimba yachoropoka

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Tamthiliya ya Jua Kali maarufu kama Naira, ameeleza kwa uchungu jinsi alivyopigwa na mwanaume wake aliyemtaja kwa jina la Othman hadi kufikia hatua ya mimba ya miezi nane kuchoropoka.

Staa wa Tamthiliya ya Jua Kali maarufu kama Naira, ameeleza kwa uchungu jinsi alivyopigwa na mwanaume wake aliyemtaja kwa jina la Othman hadi kufikia hatua ya mimba ya miezi nane kuchoropoka. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Naira ameandika ujumbe huu unaosikitisha: “Asante M.MUNGU kwa hili. Naamini umeona hili nalimudu Ndio mana ukaruhusu nilipitie. Asante. Pumzika kwa Amani binti yangu,Utaishi kwenye moyo na sala zangu siku zote inshaallah. Nilikuwa Naomba siku zote nikutane na ww, Finally nimekuona lakini MUNGU hakutaka unione…. Ni mengi nimepitia magumu, Yakuumiza katika kipindi chote cha ujauzito wako lakini ulistahimili na kuwepo… Hii ilinidhihirishia kuwa ww ni binti jasiri. Sitegemea kama ungeniacha leo Any way kazi ya Mola haina makosa. Naumia kukandwa maji ya moto bila uwepo wako! Naumia kula vyakula vya mzazi ilihali sina wa kumnyonyesha. Huwa naogopa kuangalia majeneza na miili ya watu walokufa lakini leo sikuogopa, Sikuchoka kuukumbatia mwili wako na kuubusu kila mahali. ALLAH SIKUKUFURU ASANTE”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live