Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naira Marley atishia kumshtaki muigizaji Iyabo kisa Mohbad

Naira Marley Atishia Kumshtaki Muigizaji Iyabo Kisa Mohbad Naira Marley atishia kumshtaki muigizaji Iyabo kisa Mohbad

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Naira Marley ametishia kumshtaki muigizaji kutoka nchini humo Iyabo Ojo kwa madai ya kumchafua kwa kuchapisha habari za uongo kipindi akikabiliwa na tuhuma za mauaji ya aliyekuwa msanii Mohbad.

Naira ameweka wazi kuwa atamshtaki muigizaji huyo kwa fidia ya dola 632,807 ambazo ni zaidi ya tsh 1.5 bilioni, iwapo hatomuomba msamaha kwa alichokifanya.

Naira Marley akiwakilishwa na wakili wake Olalekan Ojo (SAN) na Co, amemuandikia barua Iyabo barua, akimshutumu kwa kuchapisha maudhui ya uongo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aidha, wakili huyo anayemwakilisha Naira Marley ameomba muigizaji huyo aombe msamaha kwenye akaunti yake ya Instagram na katika gazeti la kitaifa kila siku ndani ya siku 7 baada ya kupokea barua hiyo kabla hawajachukua hatua za kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live