Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nai yamkuta akitafuta mchumba, wanaume 1000 wapanga msururu

Nai Official Nai

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muuza nyago wa video za Bongo ambaye pia ni mwanamitindo, Official Nai amekutana na balaa baada ya kutangaza kutafuta mchumba huku akianika kuwa mahari yake ni kitabu cha dini tu.

Sasa taarifa ikufikie kuwa, baada ya Nai ku-post hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram, mamia ya wanaume wametiririka wakifikisha maombi kwa mrembo huyo ya kuonesha nia zao za kutaka kumuoa.

Akihojiwa na chombo kimoja cha habari, Nai amekiri kusumbuliwa na wanaume wengi wakiwemo mastaa mbali mbali baada tu ya post yake hiyo.

Mrembo huyo amedai kuwa mpaka sasa, zaidi ya wanaume 1000 amewatia block kutokana na kumsumbua huku akidai kwamba, alichogundua wanaume wengi wanapenda vya bure.

Nai amesema sasa ameghairi kutafuta mchumba wa mahari ya aina hiyo, na vitabu vya Dini atajinunulia mwenyewe.

Nini maoni yako kwa Nai?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live