Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nai: Mimi ni WCB, Harmonize nilipenda tu wimbo....

Nai: Mimi Ni WCB, Harmonize Nilipenda Tu Wimbo  Nai: Mimi ni WCB, Harmonize nilipenda tu wimbo....

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo Official Nai ameweka sawa inshu ya kuonekana kwenye ukurasa wa Instagram akifanya 'chalenji' ya wimbo wa Harmonize jambo ambalo liliibua maswali kulikoni wakati yeye anaaminika ni team WCB.

Akiwa kwenye pati ya kumkaribisha msanii mpya wa WCB, Nai aliulizwa swali hilo na mapaparazi ambapo alifafanua.

"Mimi ni team WCB lakini sidhani kama ni kosa kucheza wimbo wa msanii ambaye hayupo WCB kama nimepita mahali nikasikia wimbo nikaupenda basi nacheza na sidhani pia kama Diamond na Harmonize wana bifu kihivyo," alisema Nai.

Alipoulizwa kama atakuwa tayari kumpokea Harmonize akitokea Marekani kwenye tuzo alizoshinda hivi karibuni, Nai alijing'atang'ata maneno na kisha akasema 'no comment'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live