Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahreel ajibu Navykenzo kupotezwa na Diamond

Nahreel Aika na Nahreel

Fri, 15 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo limeonyesha kupuuzia madai kuwa wamepotea tangu kuachia kolabo yao na Diamond Platnumz, wimbo "Katika".

Memba wa kundi hilo, msanii @nahreel amepangua shuti hilo kutoka kwa shabiki mmoja ambaye aliacha komenti kwenye ukurasa wa instagram wa Nahreel, kwa kuandika;

"Diamond mbaya sana toka mfanye naye wimbo dah, hamsikiki naumia sana", Nahreel alimjibu shabiki huyo kwa kumuandikia; "Kaa mkao wa kula".

"Katika" ni kolabo iliyowakutanisha Navy Kenzo na Diamond Platnumz, ilitoka mwaka 2018.

Fahamu, Navy Kenzo kwasasa wanajiandaa kuachia album yao ya NNE baada ya kuachia Hold Me Back (2015), AIM - Above Inna Minute (2017) na Story Of The African Mob (2020).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live