Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NETFLIX yagoma kuondoa documentary ya Kanye

NET N KANYE NETFLIX yagoma kuondoa documentary ya Kanye

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kanye West alisema kuna influence kubwa sana ya wayahudi kwenye media na makampuni makubwa kwasababu ya uwekezaji wao na mara nyingi ni kandamizi, ila anafurahi kuona amegusa panapo wauma na siku zote yupo kwaajili ya kuongea ukweli.

Hasa ukiachilia mbali makampuni mbali mbali ambayo yanaendelea kuachana na Ye, Netflix wao wamesimamia mlengo wao wa kibiashara, Kampuni hiyo ya kustream Movies imekataa kuiondoa kwenye mtandao huo documentary ya Kanye West inayoitwa Jeen-Yuhs.

Netflix wamedai Hakuna sababu ya wao kufanya hivyo, Documentary haina kauli za kibaguzi, hivyo hawawezi athiri project iliyopo kwenye mtandao wao kwa maneno ya kibaguzi ya mmiliki wa hiyo project, yaliyo ongelewa nje na utaratibu wao wa kazi.

Mbali na hilo, Antonio Brown ametangaza kuendelea kuwa Rais wa Donda Sports, baada ya Aaron Donald na Jaylen Brown kuachana na Donda Sports.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live