Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NDANI YA BOKSI: P Funk anazunguka akizeeka na madini yake kichwani

60828 Pic+p+funk

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tunatokea Salasala kupitia Mbezi ya chini kukwepa foleni ya Mwenge. Kwenye mzunguko (round about) ya Kawe pale tunakutana nayo tena. Kifupi tuliruka mkojo na kutua kwenye kinyesi. Kila mtu anataka kuwahi anakoenda. Si unajua Dar ofisi nyingi ziko katikati ya Jiji. Mvua inanyesha na kufanya Dar iwe Njombe kwa muda.

Ujinga wa mvua za Daslama ni kutukosesha fahari ya macho. Huwezi kuona totoz amazing zikikatiza mitaani. Sisi wengine bila kutazama hizi mambo tunaona kama tumezikwa hai. Raha ya Jiji kubwa kama Dar ni wingi wa warembo waliovalia kimitego. Mvua za kibwege zinafanya totoz zivae masweta utadhani tupo Ifunda. Nachukia basi tu nifanyeje sasa.

Bila mvua utaviona ‘vicheche’ kwenye bodaboda vimejibinua. Vikiwahi madanga au guest. Kuna siku unalala shingo kama imewekwa zege. Kwa sababu mchana kutwa unageuka huku na huko kutazama ubora wa Mungu katika kuumba. Hiyo ni sehemu ya raha ya mji. Lakini mvua ikinyesha atapandaje bodaboda? Wanaogopa mvua kuliko AIDS.

Kwenye foleni napata muda wa kufuatilia mahojiano ya P Funk kwenye XXL. Ukitaka kujua Dozen ni mfalme wa vipindi vya mchana, sikiliza maswali yake. Ukitaka kujua akili ya P Funk, sikiliza majibu yake. Bonge moja la ‘intavyuu’. Unatamani wasimalize na hasira za foleni zikaisha. Majani anajibu swali na kuliacha ‘gemu’ wazi la muziki kama vazi la kahaba.

P Funk huyu si yule. Wa sasa unaweza usimsikie popote zaidi ya ‘biti’ zake zinapopigwa ngoma za zamani. P Funk wa zamani kila wiki alikuwa anatambulisha wimbo au msanii mpya. Bongo Fleva yote aliifanya mateka huku sikio la shabiki na ‘dijeizi’ likitegwa Bamaga. Alikuwa kiwanda kikubwa cha kuzalisha nyimbo na wanamuziki.

Burudani ni namna Majani alivyokuwa anajibu. Swali la mambo ya zamani alijibu vyema. Mambo ya ‘gemu’ la sasa alijibu vizuri. Kiasi kwamba mtu unajiuliza kajuaje kila kitu wakati kajiweka kando muda mrefu na ‘gemu’? Jamaa ni mchizi muziki, ‘intavyuu’ ili ilionyesha kuwa mchizi kafunga ndoa na muziki. Ilipendeza sana.

Pia Soma

Hapa ndipo utaona tofauti yake na wengine. Muziki haujampa ‘stress’ bado ‘anainjoi gemu’ na analihusudu. Anachotaka Majani ni usalama wa kipato chake na si kutoa nyimbo tu kama kichaa. Na usalama wa haki ya kipato chake upo Cosota. Suala la hakimiliki limehama kutoka kwenye kilio cha sanaa na wasanii. Na sasa imekuwa pambio kama pambio zingine.

Bahati mbaya walioaminiwa pale Cosota wamelala usingizi wa pono. Na wasanii wenyewe hawajui hata nini cha kufanya. Hakuna kitu kibaya kama hujui halafu hujui kama hujui. P Funk anajua na anajua kuwa anajua. Ndio maana humsikii kwenye ‘gemu’ la kutaka sifa tu za kusikika. Umri unakwenda ni wakati wa kutengeneza mazingira bora ya kina Paula.

Anachopigania P Funk hata hakimhusu maana umri alioishi ni mrefu kuliko uliobaki. Ndo ukweli. Kwa mujibu wa vitabu vya kiroho umri wa binadamu ni miaka 70. Anachofanya anajenga mazingira rafiki kwa kina Paula kama watataka kufanya muziki kama baba yao. Wasikute hali ile ile ya kudhulumiwa jasho lake.

Chidi a.k.a Chuma au King Kong. Rashid wa Ilala mbabe hasa anapopewa eneo la kughani. Mwenye mikogo na swaga za Kihip Hop. Tajiri wa sauti ambayo humbeba katika aina yake ya muziki. Sauti nzito inayokwaruza, inampa thamani anapofloo. Mbali na hilo Beenz anabaki kuwa mkali wa mitambao kwenye Hip Hop. Anajua jamaa huo ndo ukweli.

Yeye na Q Chillah, wakiwa kwenye kilele cha mafanikio. Dar es Salaam ikizunguka kupitia mbavu na koo zao. Mabega yao yakipanda juu kwa mbwembwe kifua mbele kama wamepigwa ngumi za mgongo. Wakatekwa na matumizi ya dawa za kulevya. Wakapoteza heshima na umaarufu wao, baada ya kugundulika.

Wakapoteza biashara yao na kuanza kuhangaika namna ya kurudi upya sokoni. Biashara ikawa ngumu kuuzika baada ya kupewa kisogo na soko la muziki. Yakiwa ni matokeo ya kubwia unga. Chillah ni muda mrefu sasa tangu atangaze kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

Inavutia kwamba aliamua kuacha mwenyewe. Hakwenda kwenye vituo vya msaada na dawa za kuwezesha kuachana na uteja (rehab). Pia nyuma yake kuna stori nzuri yenye kuvutia. Kwamba Chillah aliwatazama watoto wake na kujiona siyo baba bora. Kwa kugeuka mteja wa dawa za kulevya. Mchizi akapiga chini mondo.

‘Muhuni’ wa Ilala, alitangaza kuachana na dawa za kulevya na kurudia. Kimsingi alionekana kuumizwa na dawa za kulevya ila sumu ilimzidi nguvu mwilini. Alienda rehab na kutoka na ahadi nyingi kuwa amepona na hatorudia tena lakini baada ya muda akavunja ahadi yake. Alikuwa na nia, lakini nia ikazidiwa na vishawishi.

Chillah hajapoteza sauti yake, anaimba vizuri, amekomaa kuliko wa Smooth Vibes kwa Ruge Mutahaba. Hivi sasa anateswa na mazingira. Mbona hafanikiwi? Ni kweli kuna muda aliupoteza katikati alipozamia kwenye unga, lakini mbona amejirekebisha na bado mafanikio hayaoni? Ukiuvaa uhusika wake utaelewa mateso haya ndani yake. Anawaona kina Diamond, Kiba na wengine wanatengeneza pesa kwenye muziki, halafu anaumia kwa ndani. Chillah anaona wote hao hawamuwezi kikazi. Hawamuwezi kwa muda alioutumia kuujenga muziki wa Kitanzania na thamani yake kwa jumla. Wote hao hakuna mwenye kuifikia gharama ya maumivu aliyopata.

Leo hii Chillah anaomba nafasi atambulishe ngoma mpya. Wakati hadhi yake ni kutafutwa, watangazaji waombe kumhoji. Hapo inabidi uwaweke na TID, Daz Nundaz, Banana Zorro, Nurueli, MB Dog na wengine wengi, ambao wamefanya kazi kubwa na bado wanadai pesa nyingi kwenye muziki. Lakini wanapewa kisogo kama vile hawapo.

Ndo kitu kinachomuumiza sasa na siyo dawa za kulevya. Na bahati mbaya watu wako ‘bize’ na dengue mara kipindupindu. Matukio na mikasa ni mingi kiasi kwamba ili ukimbize kwenye ‘gemu’ lazima uwe na kitu cha ziada. Chillah bado ana imani ile ile ya zamani. Kutengeneza wimbo, kuusambaza na kufanya mahojiano.

Lakini WCB wanaanza na lawama za ‘penzi feki’ la ‘Mwarabu Faita’ na Sarah. Watu wanatega sikio kumbe ujio wa ngoma mpya. Wakati Chillah anabadilika kutoka kwenye matumizi ya dawa za kulevya. Muziki nao unabadilika kwenda kwenye kutegemea kiki zaidi ya ubora wa ngoma.

Ngoma ya Muda ni kali. Lakini Chidi wa Muda amepungua kwa kumlinganisha na Chid wa Dar es Salaam Stand Up, ingawa floo bado ni ileile. Anawaona kina Bilnass na wenzake wanatengeneza pesa wakati yeye mkali zaidi yao hapati kitu. Anaumia sana, ndiyo maana anasema Muda wake na gharama za maumivu aliyopata hawawezi kumfidia.

Chidi na Chillah wakililia ‘intavyuu’ au ‘eataimu’. P Funk yeye anazeeka akizunguka na madini kichwani. Anaudai muziki kwa kiasi kikubwa. Kwa bahati nzuri yeye anajua tatizo ni nini tofauti na kina Chillah. Ndo maana kakaa kando mpaka mambo yakae sawa. Hataki kujitia stress ya kutengeneza kitu kikali na kutopata kile anachostahili.

Katumia muda mwingi kujenga muziki na wanamuziki. Katumia muda mwingi kuburudisha watu. Lakini alichoingiza kwa muda wote hakistahili. Huu siyo wakati wake wa kuwaza ndinga, hizo ni nyakati za kina Lizer, DaxoChali na wenzao. Hataki kuona kina Paula wanaingia kwenye ‘gemu’ likiwa na makando kando ya ukosefu wa hakimiliki kwa msanii.

Sugu, Prof Jay, Gangwe Mob, Juma Nature, Wagosi wa Kaya, Jaymoe, AY, FA, Afande Sele, Mr Nice, Dudubaya, Lady Jaydee, Stara Thomas na wengine. Katika namna ile ile, hakuna wa kufidia muda na maumivu ya gharama waliyobeba. Muhimu tu ni kuwapa heshima. Lipo daraja wanalostahili. Tusiwachukulie poa, wakati ni wao waliofanya muziki ukawa na thamani.

gi miaka ya karibuni wanakimbilia kwa ‘watumishi’, maaskofu na wachungaji kuombewa. Kinachowapeleka wengi wao ni kupata mume, ndoa au mimba. Haya nd’o matatizo makubwa ya dada zetu. Na matatizo haya umekuwa mtaji mkubwa kwa makanisa mengi ya kiroho.

Nataka kumaanisha nini? Kwamba kisiwe kitu cha ajabu watumishi kukutwa na janga kama hili. Na huyu amekuwa mhanga wa ‘skendo’ hizi kwa sababu siyo mara ya kwanza. Huwezi kuvuna njegere kwenye shamba ulilopanda kunde. Waumini wao wengi ni kinamama.

Jitu linaendekeza mipombe, bange na kila aina ya ulevi kiasi kwamba linashindwa kutimiza wajibu wake kwa mkewe.

Mwanamke anajua karogwa nd’o maana hapati mimba anaamua kwenda kwa watumishi wamuombee. Kumbe hana tatizo lolote bali mume ndiye anayehitaji maombezi.

Wasichana wengi wanaishi maisha ya kimjinimjini sana. Asubuhi yuko baa anapata supu, mchana yuko saluni kwenye umbea. Usiku yuko baa kwenye mitungi. Muda wote anakoleza marangi usoni akiamini ndiyo mvuto wa kupata mume. Anageuzwa kifaa cha starehe tu.

Kuna miaka kati ya 18 mpaka 25. Hapo msichana akipoteza mwelekeo wake basi imetoka hiyo. Kuanzia hapo wengi huishia katika ‘usingo mamaz’ kwa kuzaa na yeyote. Mpaka unafikisha miaka 25 unatakiwa kuwa na bwana mwenye miaka 35 na kuendelea.

Usianze kusaka bwana sahihi baada ya kufikisha miaka 25, tafuta kabla. Kuanzia hapo kwenda juu utaishia kusumbua watumishi na waganga wa jadi. Wakati muda wa kufanya hayo uliishia kurukaruka na kudanga kama ngisi. Kosa la wengi ni katika kuzingatia muda.

Okay kwenye ile video tusimjadili yule mwanaume. Tuanze kumjadili yule ‘kicheche’ tunamuita ‘kicheche’ kwa sababu ni ‘kicheche’ pekee anayeweza kurekodiwa kibwege namna ile kwenye lile tendo. Mwenye akili timamu hawezi kukubali.

Kwa uzuri ule hawezi kukosa kuwa na mume, mchumba au bwana’ake wa uhakika. Kwa lile umbile, rangi na sura ni dhambi kukosa bwana sahihi wake wa pekee. Mana’ake nd’o wale wasichana wanapoteza dira na mwelekeo kwenye miaka 18 mpaka 25. Wako wengi.

Muda wa kutulia na bwana mmoja na sahihi wanadanga ili wavae nguo mpya kila wiki, walewe na kubadili nywele zao.

Muda wa kusoma wako ‘bize’ mitandaoni kufuatilia maisha ya mastaa ambao asilimia tisini wamefeli maisha ndipo wakajiingiza kwenye uigizaji na muziki.

Haya matukio yanazalisha wadangaji na ‘usingo mamaz’ pia kwa kiasi fulani huletwa na wadangaji. Wadangaji huvuruga ndoa, penzi na uchumba. Kifupi ni kwamba kwa kiasi kikubwa chanzo cha ‘singo mamaz’ pia ni ‘singo geloz’ ambao hawataki uhusiano sahihi zaidi ya kudanga.

Uzinzi siyo kwamba unaharibu ndoa, familia na maisha tu, lakini huharibu roho na roho kwa njia inayosababisha kifo cha kimwili na kiroho.

Mungu anatamani kwamba tuwe bila hatia na tutumie miili yetu kama zana za matumizi na utukufu wake. Mwili siyo kwa uzinzi bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.

Ingawa uzinzi ni dhambi, makahaba hawajazidi upeo wa Mungu wa msamaha. Biblia inaonyesha matumizi ya kahaba aitwaye Rahabu ili kuendelea na kutimiza mpango wake. Kwa sababu ya kutii kwake, yeye na familia yake walitunukiwa na kupewa baraka.

Yote kwa yote ile video tusimame kwenye ukweli, kwamba urembo wa yule ‘dem’ lazima shetani achukue pointi zote tatu ugenini.

Chanzo: mwananchi.co.tz