Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

NASA yataja mwanamke wa kwanza na Mwafrika wa kwanza kwenda mwezini

Nasa 6932feb NASA yataja mwanamke wa kwanza na Mwafrika wa kwanza kwenda mwezini

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la anga za juu la Marekani Nasa limewataja wanaanga wanne ambao watarudisha shughuli za binadamu kwenye Mwezi, baada ya pengo la miaka 50.

Christina Koch atakuwa mwanaanga mwanamke wa kwanza kuwahi kutumwa kwa misheni ya kwenda kwenye mwezi, huku Victor Glover akiwa mwanaanga wa kwanza mweusi.

Wataungana na Reid Wiseman na Jeremy Hansen kuendesha chombo kuzunguka Mwezi mwishoni mwa mwaka ujao au mapema mwaka wa 2025.

Wanaanga hawatatua Mwezini, lakini misheni yao itafungua njia ya kuguswa na wafanyakazi wafuatao.

Raia hao watatu wa Marekani na Mkanada mmoja waliwasilishwa kwa umma katika hafla iliyofanyika Houston, Texas.

Sasa wataanza kipindi cha mazoezi makali ili kujiweka tayari.

Katika kuchagua mwanamke na mtu wa rangi, Nasa inatimiza ahadi yake ya kuleta utofauti mkubwa katika juhudi zake za uchunguzi.

Misheni zote za hapo awali za wafanyakazi kwenda Mwezini zilifanywa na wazungu.

Reid Wiseman (47): Rubani wa Jeshi la Wanamaji la Marekani ambaye alihudumu kwa muda kama mkuu wa ofisi ya mwanaanga ya Nasa. Ameendesha safari moja ya awali ya kwenye anga, hadi kituo cha anga za juu cha Kimataifa mwaka wa 2015.

Victor Glover (46): Rubani wa majaribio ya Jeshi la Wanamaji la Marekani. Alijiunga na Nasa mwaka wa 2013 na kufanya safari yake ya kwanza ya anga mnamo 2020. Alikuwa Mwafrika wa kwanza kukaa kwenye kituo cha anga za juu kwa muda mrefu wa miezi sita.

Christina Koch (44): Mhandisi wa umeme. Anashikilia rekodi ya muda mrefu zaidi angani na mwanamke, ya siku 328. Akiwa na mwanaanga wa Nasa Jessica Meir alishiriki katika matembezi ya kwanza ya anga ya juu ya wanawake wote mnamo Oktoba 2019.

Jeremy Hansen (47): Kabla ya kujiunga na Shirika la Anga za Juu la Canada, alikuwa rubani wa kivita katika Jeshi la Wanahewa la Canada. Bado hajawahi kwenda kwenye anga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live