Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

“Mzungu karibu anitoe roho, kilinichoma!” Akothee ajutia ndoa yake

Akothee Na Mzungu.png “Mzungu karibu anitoe roho, kilinichoma!” Akothee ajutia ndoa yake

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mwimbaji na mfanyabiashara mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee hivi majuzi alishiriki katika kipindi cha moja kwa moja kwenye Tiktok na meneja wake Nelly Oaks.

Katika kipindi hicho cha moja kwa moja, Nelly Oaks alionekana jikoni akimuandalia chakula mwimbaji huyo ambaye alikuwa kwenye chumba cha kupumzika akizungumza naye na mashabiki.

Meneja huyo alifichua kuwa alikuwa akimtayarishia Akothee chakula maalum kwa sababu maalum.

“Kwa kweli huwezi kuja jikoni. Hii ni chakula cha jioni maalum kwa mtu maalum kama wewe. Ni surprise,” Nelly Oaks alisikika akimwambia Akothee alipoomba kwenda kumsaidia jikoni.

Katika kipindi hicho, mama huyo wa watoto watano alisikika akimuita Nelly Oaks ‘bae’ mara kadhaa, jina ambalo hutumika sana na wapenzi.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 pia alisikika akijigamba kuhusu mapenzi ya Nelly Oaks kwake na pia kukejeli ndoa yake iliyovunjika na Denis ‘Omosh’ Schweizer.

“Ni vizuri sana kupendwa, nilikuwa nimeenda huko (to Schweizer) nikifikiria ni , ati greener pastures, kimenichoma!!.. Ati mzungu wueh! Kumbe mzungu!,” Akothee alisema.

Aliendelea kuzungumzia masaibu yake na aliyekuwa mume wake mzungu akisema, “Mzungu karibu anitoe roho, nitakuja kuwaelezea siku moja.”

Katika kipindi hicho, Akothee pia aliwazima vikali wanawake waliokiri kuvutiwa na meneja huyo wake akisema kuwa tayari amempata na hayuko tayari kwao.

Mwimbaji huyo kwa kejeli aliwataka wanawake hao badala yake wamtafute aliyekuwa mumewe, Denis Schweizer akibainisha kuwa mzungu huyo kwa sasa hana mchumba.

“Kwa nini mnang’ang’ania na Nelly Oaks. Si muende mchukue Omosh, muende mchukue Omosh wa Pakistan. Yeye ndiye ako single,” alisema.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya mama huyo wa watoto watano kuthibitisha kugonga mwamba kwa ndoa yake na mzungu huyo kutoka Uswizi.

Chanzo: Radio Jambo