Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mzungu ajibadili rangi kwa kuutamani U-afrika

Martina Big Martina Big na mumewe

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tumezoea kuona baadhi ya watu wenye rangi nyeusi kujibadili rangi ya ngozi kwa kujichubua ili wawe weupe, hiyo ni tofauti kwa Martina Big, raia wa Ujerumani ambaye alichukua uamuzi wa kubadili rangi ya ngozi yake kutoka kuwa mweupe hadi kuwa mweusi.

Inaelezwa kuwa kutokana na kuvutiwa na ngozi nyeusi, mwaka 2017 Martina alianza kuchoma sindano za kubadili rangi ya ngozi yake hadi kufikia rangi nyeusi , huku akichoma sindano nyingine za kuongeza matiti yake ili yawe makubwa kwa kuamini kuwa atakuwa na muonekano wa kiafrika Mara kadhaa alibadili nywele zake na kuzifanya ziwe ngumu.

Baada ya kukamilisha jambo lake na kupata ngozi nyeusi Martina alihamia nchini Kenya yeye na mumewe sasa anatambulika kama raia wa Kenya baada ya kupewa uraia wa nchi hiyo, amepatiwa jina la kiafrika ambalo wanamuita Malkia Kubwa. Martina ameshachoma sindano zaidi ya 20 ili kubadili muonekano wake, alizaliwa mwaka 1988 anajishughulisha na uigizaji.

Kwa mujibu wa Daktari wa Martina ni kuwa, kutokana na sindano alizochoma anaweza akapata watoto wenye ngozi ya rangi nyeusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live