Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzombe Mahamoud anayeigiza sauti ya Sumbul Aga

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kuhusu Sumbul Aga

Jina lake halisi ni Selim Bayraktar, ni Mturuki mwenye asili ya Iraq aliyehamia Uturuki baada ya kuuawa kwa Saddam Hussein ambapo vijana walikuwa wakienda kuchukuliwa shuleni kwa ajili ya kujiunga na jeshi.

Hata hivyo familia yake haikutaka awe mwanajeshi na hivyo kumhamishia Uturuki na huko alijiunga na Chuo cha Sanaa cha Hecettepe na nyota yake ya usanii ikaanza kuchipukia hapo.

Mzombe Mahamoud

Huyu ni msanii anayenakilisha sauti ya Sumbul Aga, anayesema anafurahia kuifanya kazi hii ambayo ilikuwa ni moja ya ndoto zake.

Anaeleza kuwa licha ya watu kumwambia amemtendea haki Sumbul Aga, hata yeye anajikubali anapoigiza sauti ya msanii huyo kivutio kwenye tamthilia ya Sultan.

Anasema maoni anayopata kwenye jamii anaamini yanadhihirisha kuwa ameuvaa uhusika wa nafasi aliyonakilisha sauti.

Akimwelezea Sumbui anasema ni mtu ambaye anapenda fedha pindi anapokutumikia kwa jambo lolote na kama huna utaishia kumungalia kwa macho.

Mbali na kunakili sauti katika tamthiliya mbalimbali zinazoonyeshwa Azam Tv, Mahamoud alishaigiza vichekesho vya Jambo na Vijambo, filamu ya T –Junction, Going Bongo, Shoe Shine na pia ni mwigizaji mzuri wa majukwaani.

“Yaani ukinikuta majukwaani utanisahau kwani huku ndipo nakotamba zaidi japokuwa bado Watanzania hawajaielewa vizuri sanaa ya majukwaani,” anasema.

Kuhusu malengo yake anasema ni kuwa mnakilishaji wa sauti wa kimatiafa na mwigizaji mkubwa nchini.



Chanzo: mwananchi.co.tz