Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Mzee wa Upako: Ni ngumu mwanaume kukosa mchepuko

MZEE WA UPAKO Mzee wa Upako

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako amesema kuwa kisaikolojia ni vigumu kwa mwanaume kukosa mchepuko hivyo wanaume wengi wanatoka nje ya ndoa zao.

"Mwanaume asilimia kubwa hata akiwa na mwanamke nje hana maana kwamba hamtaki mke wake aliyemuoa na kumuweka ndani, ni ngumu sana kukuta mwanaume ambaye hana mchepuko ni kitu cha nadra sana, ukichukua wanaume 100 wanaume 90 lazima wanachepuka.

"Hii inatokana na kwamba, kwanza mwanamke anazeeka haraka, ila mwanaume hazeeki, mwanaume anaweza kuzalisha hata akiwa na miaka 100 lakini mwanamke akifikia tu ukomo wa hedhi hawezi kuzaa tena na hiyo ni sheria aliyoiweka Mungu.

"Kwa hiyo usishangae swala la mume wako kuchepuka, ni kawaida maana hata wanyama huko porini wanachepuka, hawakai na mwanamke mmoja," amesema Mchungaji Anthony Lusekelo, Mzee wa upako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live