Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee wa Mjegeje alisema maiti yake itagoma kuzikwa Bagamoyo

Mzee Wa Mjegeje Mzee wa Mjegeje enzi za uhai wake.

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Thabiti Ally Kipwasa ‘Real Jimmy’ ambaye ni Meneja wa aliyekuwa msanii wa Bongo anayefahamika kwa jina la Omar maarufu kama Mzee wa Mjegeje amefunguka kwamba kabla msanii huyo hajafariki, alisema ndugu zake wasihudhurie mazishi yake maana hawakumsaidia kipindi anaumwa.

Thabiti ameongeza kuwa, Mzee wa Mjegeje alitoa kauli kuwa akifa asizikwe nyumbani kwao Bagamoyo, badala yake azikwe Dar es Salaam kwa sababu ndugu zake wote walimkataa enzi za uhai wake.

Mzee wa Mjegeje aliyetamba kwenye mitandao ya kijamii kwa video yake ya 'Kata simu tupo site' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Machi 20, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matoiabu.

“Hatujafikia mwafaka wowote mpaka sasa, kwa sababu mimi na mama yangu ambaye ni mama Kipwasa (Mjumbe) lakini ndugu walimkataa labisa.

“Mzee aliniambia kuna ndugu yake mmoja tu anaitwa Shaidi, huyo ndiyo utakaa naye kujua mimi nazikwa wapi lakini msinipeleke bagamoyo, nizikeni dar es salaam kwa sababu ndugu zangu wote wamenikataa.

“Sasa leo wanakuja watu ambao siwajui, namjua mmoja ambaye nasikia sauti na leo amekuja nikahakiki kuwa ni yeye.

“Mara ya mwisho nampa mzee uji saa saba kasoro uaiku alikuwa akiongea kwa tabu sana, nikamwambia utapona akaniambia Thabiti naomba msinipeleke Bagamoyo.

“Alitamka kauli kuwa ndugu zake wasihudhurie kwenye mazishi yake, hata wakinipeleka Bagamoyo mimi sitaenda nitakatagoma,” amesema Thabiti.

Mzee wa Mjegeje alikuwa msanii kutoka Bagamoyo, Tanzania ambaye alikuwa akijihusisha na shughuli zote za sanaa hasa za maigizo ya vichekesho na uimbaji wa muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live