Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Yusuf kumpa mkataba mkewe

7ccc195bd4d8781ea414fe5df609ef75 Mzee Yusuf kumpa mkataba mkewe

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII nguli wa taarabu, Mzee Yusuf, ambaye amerejea kwa kishindo katika muziki huo, amesema yupo mbioni kuwapa mikataba ya kazi wasanii wake wote akiwemo mkewe.

Mzee Yusuf hivi karibuni alirejea katika taarabu baada ya kuwa kando kwa takribani miaka minne, akijihusisha na nyimbo za kaswida na alikwenda kuhiji Makka ili kutekeleza moja ya nguzo za Waislamu, ambapo baada ya kurudi alisema anaachana na muziki huo ili amtumikie Mungu.

Alisema hivi karibuni atatangaza wasanii wake na kila mmoja atapatiwa mkataba wa kazi, ili kundi hilo lifanye mambo yake vizuri. Katika mahojiano na mtandao mmoja hivi karibuni, msanii huyo alisema atafanya ziara katika mikoa mingi kama Morogoro, Dodoma, Rukwa na mingine ikiwa ni muendelezo wa yeye `Kurejea Mjini’.

Mzee Yusuf aliibuka na `Kurudi Mjini’, ikiwa ni hatua yake ya kurudi katika muziki wa taarabu alioacha kwa miaka kadhaa.

Chanzo: habarileo.co.tz