Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Abdul: Mimi na Diamond tuko vizuri

Baba Diamond Mzee Abdul: Mimi na Diamond tuko vizuri

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba wa supastaa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Mzee Abdul Jumaa amesema kuwa ameshamaliza tofauti zake na familia ya Diamond hivyo kwa sasa yupo sawa na mwanaye huyo.

Itakumbukwa kuwa, miaka kadhaa iliyopita familia ya Diamond ilidai kuwa baba mzazi wa msanii huyo si mzee Abdul kama watu wanavyojua, badala yake baba wa Diamond ambaye aliitwa Mzee nyange alishafariki Dunia.

"Mimi na Diamond Platnumz tuko vizuri, bado ni mwanangu yeye anaitwa Naseeb Abdul mimi naitwa Mzee Abdul, tuko vizuri hadi familia yake ingawa kuna kipindi nilikasirika baada ya mama yake kuleta mambo ambayo hayakuwa ya kweli.

"Diamond na Queen Darleen wote ni watoto wangu, sina shida nao na hata nikiwa na shida hawawezi kunitupa," amesema Mzee Abdul.

Aidha, Mzee Abdul amesema ameacha kuimba muziki kwa sababu umri wake haumruhusu, ameshachelewa hata akisema aimbe vipi hataeleweka, lakini moja ya vipaji alivyojaliwa na Mungu ni kuimba na kuigiza na hata watu wa Tamthilia za Juakali, Huba, Pazia na nyinginezo wakimuita yupo tayari na atafanya vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live