Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzazi mwenzie Steve Nyerere atoa siri ya kubadili dini

73594 Dini+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wellu Sengo, mzazi mwenzake na msanii wa filamu, Steve Nyerere ametoboa siri ya kilichomsukuma kubadili dini na kuwa Muislamu.

Wellu aliyepata umaarufu kupitia jina la Matilda ameeleza hayo leo Ijumaa Agosti 30,2019 alipozungumza na Mwananchi ikiwa ni siku moja tangu atangaze kubadili dini.

Jana katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram aliandika” Assalamu Allaykum  leo tarehe 29 Agosti 2019 mimi Wellu J Sengo  nimeslimu na kuwa Amina J Sengo, naombeni ndugu zangu katika imani mnishike mkono.”

Amesema baba yake ni Muislamu, mama yake hakuwahi kumbana afuate dini ipi.

 “Mama yangu aliniambia nitakapokuwa mkubwa na kujitambua hatanizuia kubadili dini kwa kuwa hayo yatakuwa ni maamuzi yangu. Kutokana na kutowekewa kizuizi na mama yangu nimeona kwangu huu ni muda mwafaka wa kufanya hivyo, ”amesema.

 

Pia Soma

Advertisement   ?

Chanzo: mwananchi.co.tz