Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzazi mwenza aanika siri nzito za Mbosso

Mbosso Rcuky.jpeg Mzazi mwenza aanika siri nzito za Mbosso

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmoja wa wazazi wenza wengi wa Mbosso, Rukia Rucky almaarufu Mama Ikram amefunguka kuhusu kipindi cha mahusiano yake na msanii huyo.

Mbosso na Rukia waliingia kwenye mahusiano takribani miaka mitatu iliyopita na wakajaliwa mtoto wa kiume mnamo Agosti 2019.

Rukia amefichua kuwa msanii huyo wa WCB alimnyemelea na kumtongoza kupitia mtandao wa snapchat.

"Baba Ikram alianza kunitext snapchap. Tumeseji tukaanza urafiki kidogo baadae ndo tukaanza kuwa na mahusiano," Mama Ikram alisema katika mahojiano na Wasafi Media.

Mrembo huyo ndiye mpenzi wa mwisho wa Mbosso anayejulikana wazi.

Rukia alifichua kuwa staa huyo wa anamthamini mapenzi ya mkweli, asiye na marafiki wengi na anayewekeza muda na mtoto wake.

"Ni baba anayependa muda wote uwe na mtoto wake, anapenda sana mtoto wake, hata anaweza asikuone wa maana kama hushughuliki na mtoto wake," alisema Rukia.

"Mbposso ni mtu ambaye anapenda kusikiliza maneno ya watu, akiambiwa kitu kidogo anapatwa na wasiwasi,"

Alieleza kuwa msanii huyo hukasirika wakati mwenzake anapokuwa hapokei simu ama kutokuwepo nyumbani anapotembelea mwanawe. Pia, alifichua kuwa staa huyo wa Bongo anapenda sana kudekezwa na kubembelezwa na mpenzi wake.

"Mimi ni mtu ambaye napenda kujishusha, nikikosea naomba msamaha. Nilikuwa nikiomba msamaha, anapenda sana kubembelezwa. Sasa nikikosea nambembeleza bembeleza, 'Mbosso nisamehe'.." Alisema.

Rukia alifichua kuwa Mbosso Platnumz hupata ndoto za kiajabu mara nyingi akiwa usingizini. Aidha, aliendelea kueleza kuwa mzazi mwenzake huyo anapenda sana kupikiwa ubwabwa kwa maharage au samaki.

"Ukimpikia ugali usiku anakwambia huwa anaota ndoto mbaya akila. Hata mchana labda awe na hamu na huo ugali ndio ale. Anapenda tu ubwabwa," alisema Rukia.

Ingawa idadi halisi ya wanawake ambao amewahi kupata watoto nao haijulikani, Mbosso kwa kawaida huwa hafichi ukweli kuwa yeye ni baba wa watoto wengi. Hata hivyo ameonekana kumpendelea zaidi Rukia na ambaye ni mama ya mtoto wake wa mwiisho anayejulikana, Ikram.

Hivi majuzi mwanamuziki huyo akiwa kwenye mahojiano alidokeza kuwa bado ana hisia kubwa kwa Rukia huku akibainisha pia kuwa amezaa na aliyekuwa mke wa msanii mwenzake, Abdu Kiba.

"Nafasi ya Mama Ikram katika moyo wangu ni kubwa sana kwa sababu kipindi nilikuwa naanza sanaa alikuwa ananisapoti sana. Mama Ikram ni special," Alisema katika mahojiano.

Aliongeza kuwa mtoto ambaye alipata na Bi. Rukia ni ,"Mwanangu wa dhahabu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live