Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mwanamuziki MohBad wafukuliwa Nigeria

Mwili Wa Mwanamuziki MohBad Wafukuliwa Nigeria Mwili wa mwanamuziki MohBad wafukuliwa Nigeria

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Mwili wa nyota wa Afrobeats wa Nigeria MohBad umefukuliwa, polisi katika jiji la Lagos walisema.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye jina lake halisi lilikuwa Ilerioluwa Aloba, alifariki Jumanne Septemba 12 katika hospitali ya Lagos.

Mazingira kamili ya kifo chake hayajawekwa wazi na kumekuwa na swito kutoka kwa mashabiki wake kwa uchunguzi.

“Ufukuaji umekamilika. Uchunguzi wa maiti utaanza," msemaji wa polisi wa jimbo la Lagos Benjamin Hundeyin alitweet.

Tangu kifo cha mwanamuziki huyo kumekuwa na mikutano katika miji ya kusini mwa Nigeria na huzuni nyingi ikitanda huku watu wakitaka majibu. Hashtag #justiceformohbad imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii.

Mwimbaji marehemu alikuwa maarufu kwa sauti yake ya baritone na nyimbo zake zikiangazia masuala ya mitaani , wakati mwingine masuala machafu.

Chanzo: Bbc