Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa msanii nyota wa DRC haujazikwa miezi saba baada ya kifo chake

Mwili Wa Msanii Nyota Wa DRC Haujazikwa Miezi Saba Baada Ya Kifo Chake Mwili wa msanii nyota wa DRC haujazikwa miezi saba baada ya kifo chake

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Familia ya mpiga gitaa maarufu wa DR-Congo Lokassa ya Mbongo inasema inapitia "maumivu yasiyomithilika" na "fedheha" huku wakisubiri usaidizi wa serikali kumzika karibu miezi saba baada ya kifo chake.

Mwili wa Lokassa umelazwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kinshasa baada ya kusafirishwa kwa ndege kutoka Marekani kwa mujibu wa matakwa yake ya kuzikwa nchini mwake.

Mwanawe André Marie Lokassa aliambia BBC kwamba serikali iliahidi kusaidia kuandaa mazishi ambayo "itastahili" jina la nyota huyo wa muziki, lakini hadi sasa imeshindwa kufanya hivyo.

Shirika la msaada kwa wasanii, hata hivyo, lilisema kuwa migogoro ndani ya familia ilisababisha hali hiyo.

Afisa wa mawasiliano katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi, Magloire Paluku, alikataa kutoa maoni yake alipopigiwa simu na BBC, akielekeza maswali kwa familia.

Bw Lokassa aliambia BBC kwamba familia hiyo iliwasilisha ombi la bajeti ya dola 75,000 (kwa serikali kwa ajili ya gharama za mazishi, lakini bado halijaidhinishwa, na kuacha familia katika sintofahamu.

"Inasikitisha na kufedhehesha, naweza kusema hivyo," Bw Lokassa alisema, akiongeza kuwa kucheleshwa kwa mazishi hayo kunasababisha mvutano katika familia.

Chanzo: Bbc