Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa msanii aliyekufa wasimamishwa wima ili mashabiki wamuage

Saniiiii 2pm 24331 Mwili wa msanii aliyekufa wasimamishwa wima ili mashabiki wamuage

Sat, 2 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara nyingine tena raia wa Ghana wamezua gumzo katika mitandao ya kijamii kuhusu utamaduni wa kuaga marehemu.

Kisa cha kushangaza ambacho kimezua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii ni baada ya mwili wa msanii mmoja aliyefariki kwa ajali wiki iliyopita ulivyoagwa na umma na mashabiki wake.

Katika picha na video ambazo zimeenezwa kwenye mitandao ya kijamii, rapa huyo kwa jina 2pm alitolewa mochwari na kufikishwa nyumbani kwake lakini kabla ya maziko, mashabiki wake wakataka kumuaga mara ya mwisho kwa kuutazama mwili wake wote.

Kwa kawaida katika jamii nyingi, mwili hutazawa ukiwa umelazwa ndani ya jeneza, lakini nchini Ghana hali ni tofauti; mwili wa kijana huyo uliondolewa mazima ndani ya jeneza na kuegemezwa kwa kusimamishwa wima huku watu wakipita na kuutazama utadhani ni kinyago kilichokuwa kimevalishwa nguo.

2pm alikutana na kifo chake katika ajali mbaya iliyotokea Ijumaa, Novemba 17, huko Wassa Akropong, Mkoa wa Magharibi wa Ghana.

Maiti yake ilikuwa imesimamishwa ndani ya kijumba cha glasi ukiwa umevalishwa kofia, saa, mavazi aliyopenda kuvalia, cheni kifuani lakini pia fimbo mkononi, kwa mbali ungedhani ni kinyago cha kuuza nguo Kariakoo kumbe ni maiti.

Nini maoni yako, unaona hii ni sawa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live