Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mchekeshaji Erick Kisauri waagwa Kibaha

Erick Kisauti Kuaga Mwili wa mchekeshaji Erick Kisauri waagwa Kibaha

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa aliyekuwa msanii maarufu wa vichekesho, Zabogan Zabron maarufu kama Erick ‘Hivyo Hivyo’ ama 'Erick Kisauti' umeagwa Kibaha, Kwa Mathias mkoani Pwani.

Erick ambaye alifariki dunia alfajiri ya jana Agosti 17, 2022, mwili wake unasafirishwa leo jioni kwenda nyumbani kwao Mwanza ambapo maziko yanatarajiwa kufanyika kesho Agosti 19, 2022 jijini humo.

Wasanii na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa Erick ambapo imeelezwa kuwa mpaka sasa changamoto kubwa ni kukosekana kwa pesa ya kukodisha gari kwa ajili ya kusafirisha mwili huo.

Wadau mbalimbali wameombwa kuendelea kutuma michango kupitia namba ya Mchekeshaji Tin White ambayo ni 0782281249 jina ni Masudi Jumanne, ili kufanikisha zoezi la kukodi gari na kuusafirisha mwili wa marehemu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live