Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku asimulia Harmonize anavyowachanganya Kajala na Paula

Mwijaku, Kajala Na Paula Mwijaku asimulia Harmonize anavyowachanganya Kajala na Paula

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji asiyeishiwa vituko Bongo, Mwijaku amesema anachukizwa na tabia ya Harmonize kuwachanganya Kajala na mwanaye Paula kwa mawasiliano.

Mwijaku amesema, kwa nyakati tofauti amemueleza Harmonize aache mazoea na Paula kwani sasa hivi wako kwenye mahusiano mazuri na mama yake.

“Kuna siku tulikuwa tunaenda mjini, Kajala akapiga akataka zawadi ya ice cream, wakati tunaenda kununua Paula naye akampigia akasema anataka zawadi,” alisema Mwijaku.

Mwijaku anasema walilazimika kumzuga Kajala kuwa wanapelekea nguo Kiz Daniel aliyekuwa amekuja kufanya shoo Bongo kisha wakamtuma Duke (mtu wa karibu na Harmonize) apeleke zawadi kwa Paula.

Mwijaku anasema baada ya tukio hilo, siku ya tatu yake, walikuwa wanachoma nyama nyumbani kwa Harmonize ndipo alipomfuma tena Harmonize akimkonyeza Paula kama kumsifia.

“Nilimwambia Harmonize aachae maana yule ni binti halafu yeye alikuwa amevaa tu bukta, yupo kifua wazi nikasema unamkonyeza wa nini na ni binti yako ambaye anaujua utupu wako? Harmonize alinimaind akanimbia kama unaondoka ondoka,” alisema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live