Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku amwangukia Ommy Dimpoz "Tusamehe"

Mwijaku Ommy Dcc Mwijaku amwangukia Ommy Dimpoz "Tusamehe"

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa Clouds Media, Burton Mwemba 'Mwijaku' amemwangukia kwa kumuomba radhi msanii Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' baada ya kumuibua baba yake na kudai kuwa mwanaye huyo amemtelekeza wakati yeye akila bata Ulaya.

Kauli hiyo ilimuibua Ommy Dimpoz na kuwatolea uvicu Clouds huku akisema kuwa hataki kuhusishwa na baba yake kwani alimtelekeza tangu akiwa mtoto jambo ambalo hata Mwijaku anafahamu.

"Kabla maharagwe hayajaiva huchambuliwa kwanza, ambapo maharagwe yaliyo mabovu hutupiliwa mbali ili yale mazuri yaweze kuliwa.

"Hata hivyo, mvua inapokuja yale maharagwe yaliyotupwa nje kwa kuonekana mabovu hugeuka na kuwa mbegu, humea na ikikuwa hugeuka kuwa maharagwe mazuri tena.

"Na yule aliyeyajaji kuwa ni mabaya na kuyatupa huenda yatakapo komaa atayavuna na kuyala kwa afya.

"Kupitia Ommy Dipoz, nimejifunza na maisha ndivyo yalivyo, unaweza kutengwa ukasemwa ukadharauliwa na kuumizwa vibaya na wale uliowaamini. Lakini je! ni nani ajuae njia za Mwenyezi Mungu?

"Haohao waliokuumiza itatokea siku watakutazama wakitegemea la kheri kutoka kwako, huenda watakugia magoti wakihitaji neno lako moja tu wapone.

"Usijipe laana, usihuzunike wala usilie pale dunia inapokuegemea ni swala la muda tu kupata mavuno yako ya baraka!

"Mazungumzo yangu na mzee Nyemo hayakuwa na lengo la kuharibu emage yako hata mara moja, najua story vizuri nia yangu ni kumpa furaha mzee.

"Kupitia video yako nikwambie tu. Your germination moment is just around the corner! Pray, believe and Receive, God bless y'all," amesema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live