Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku amwangukia Masoud Kipanya

Kipanyazzz (5).jpeg Mwijaku amwangukia Masoud Kipanya

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji na muamasishaji wa mambo mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii Burtoin Mwenda ‘Mwijaku’ amemuomba radhi Mtangazaji mwenziye Masoud Kipanya kwa kile alichokiongea siku za hivi karibuni.

Mwijaku baada ya kuondoka Clouds Media na kuhamia Crown Media, Masoud Kipanya alitoa maoni yake ambayo yalionekana kumkera Mwijaku.

Baada ya Masoud kuongea Mwijaku aliandika ujumbe mbaya mitandaoni kuhusu Masoud Kipanya.

Mapema leo hii mbele ya waandishi wa habari ametumia fursa hiyo kumuomba Radhi Masoud Kipanya na kusisitiza kuwa ni mtu ambaye anamuheshimu sana na ataendelea kumuheshimu sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live