Mdau wa masuala ya burudani na mwanamitandao, Burton Mwemba 'Mwijaku' amemtaka CEO wa Lebo ya Kings Music Records, Alikiba kumtimua mdogo wake, Abdul Kiba kwenye lebo hiyo kwani tayari ameshaungana na adui yao ambaye ni Diamond Platnumz.
Kauli hiyo ya Mwijaku inakuja ikiwa ni wiki chake baada ya AbdulKiba kuonekana akipari na Diamond Platnumz pamoja na wasanii wengine jambo ambalo liliibua maswali kwa mashabiki wa Kiba na Kings Music kwa ujumla.
Hata hivyo AbdulKiba alifafanua kuwa hakujua kama eneo lile Diamond alikuwepo lakini alikuja kushtuka tu baada ya kumuona akicheza wimbo wa Sumu wa Alikiba huku akidai kuwa yeye na Diamond ni washikaji tangu zamani.
"Mwiko, mwiko, nakuahakikishia tutakapomruhusu AbdulKiba kufanya kazi na mwambino tutakua tumeleta kirusi au kimea ndani ya Kings Music Records, hii ni biashara na biashara inataka ushindani.
Kama umeridhia Abdul akafanye kazi basi atoke kabisa Kings Music Records, atuache, mmbakie kua ndugu tu.
Siko tayari kuona tunaharibu biashara kisa tu Mwambino. Kwa upande wangu siungi mkono hoja. So ushauri wangu ni huo, atoke Kings Msic Records mmbakie kua ndugu, done.
Hii ni biashara akifanya mchezo tutajikuta wote tunatumika na Mwambino nazijua mbinu zake. Tumekwisha. Atakua ametimiza lengo lake la kututukana mitandaoni na kwenye media yake. Tutaweka wapi sura zetu Mfalme?," amesema Mwijaku.