Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku amshauri mke wa Baba levo "Usipigane na mchepuko"

Baba Levo Mkeweeee Mwijaku amshauri mke wa Baba levo

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa Clouds FM, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku amemshauri mke wa mtangazji mwenzake wa Wasafi FM ambaye pia ni rafiki yake, Revocatus Chipando kama Baba Levo aitwaye Salma Mdoli au Mama Ruby aache kupigana na michepuko wa mumewe, kwani kufanya hivyo ni kujishushia heshima.

Kauli hiyo ya Mwijaku inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Babab Levo kufunguka kuwa mkewe huyo amemfanyia fujo mchepuko wake aitwaye Asmah baada ya kumletea zawadi zenye tahamni ya Tsh 400,000 kutoka China huku akimletea mkewe zawadi zenye zaidi ya Tsh milioni 10.

"Sio kazi ya mchepuko wa mwanaume wako kuiheshimu ndoa yenu. Ni kazi ya mume wako kuiheshimu ndoa yenu. Kumbuka, wewe na mume wako pekee ndio mlisimama mbele ya madhabahu na kula kiapo cha ndoa.

"Acha kupigana na mtu wa nje ambaye hakuwepo wakati mnakula kiapo. Je, utapigana na wanawake wangapi kabla hujagundua kuwa Mume wako ndio haheshimu Kiapo mlichoapa?

"Haijazoeleka, lakini muda mwingine ukweli ni vizuri usemwe. Dili na mume wako. Stop fighting irrelevant parties," amesema Mwijaku.

Kwa upande wa Baba Levo yeye amesema;" Suala la kumuacha Asmah siwezi kushauriwa na Mama Ruby, ni mimi mwenyewe niamue."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live