Mtangazaji wa Clouds FM na chawa maarufu Bongo, Mwijaku, amemtaka Marioo kuwa makani na apokee simu zake mara moja kwani anafahamu atakuwa amezuiwa na Paula.
Mwijaku amesema alikutana na Marioo walipokuwa wanakwenda uwanjani kuangalia mechi ya Simba na Yanga na alimtaka kuacha mara moja tabia ya kutopokea simu zake.
"Nilimwambia kabisa ashike simu zangu, najua Paula kamzuia lakini ajue yeye ni mdodo wangu na alikuwa haachi kupokea simu zangu mimi hata mara moja, aache kabisa hii tabia," alisema Mwijaku.
Marioo na Paula kwa sasa wapo kwenye penzi motomoto baada ya mrembo huyo kuachwa na Rayvanny. Rayvanny kwa sasa amerejesha majeshi kwa mama wa mtoto wake, Fahyma.