Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku amlipua Harmonize, “anavuta bangi”

Mwijaku Na Harmo Mwijaku amlipua Harmonize, “anavuta bangi”

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chawa na mtangazaji maarufu Bongo Mwijaku, amemlipua vibaya msanii wa Bongo Fleva Harmonize huku akiweka wazi kuwa staa huyo anavuta bangi.

Mwijaku ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Bongo Five ambapo alieleza mambo mengi kumhusu bosi wake huyo ambaye kwa sasa inaonekana haziivi.

“Kuna siku nilikuwa na nyumbani kwa Harmonize, Kajala alikuwa anatuandalia chai. Sasa ikaingia meseji ya Paula, nikaiona. Nikamwambia, Harmonize usijenge mawasiliano na huyu mtoto kwa sasa maana upo vizuri na mama yake,” alisema Mwijaku.

Akizidi kusimulia maongezi yake na Harmonize, Mwijaku alisema alimwambia asiwasiliane naye maana hata kipindi cha nyuma ilikuwa hivyo hadi akamtumia picha zake za utupu lakini Harmonize akasema wakati ule alikuwa amelewa na sasa hanywi pombe.

“Kweli pombe kwa sasa ameacha lakini alikuwa amevuta bangi, nikamwambia unaweza kuandika kitu kibaya. Sijui uwezo wake wa kuihimili bangi lakini anaweza kuandika kitu kibaya,” alisema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live