Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku amburuza Nandy mahakamani

MWIJAKU MAHAKAMANI Mwijaku amburuza Nandy mahakamani

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chawa na mtangazaji wa Clouds FM, Mwijaku amemburuza staa wa Bongo Fleva, Nandy mahakamani akidai kumzulumu haki yake.

Mapema ya leo Agosti 9, 2022, Mwijaku alifika katika mahakama ya Mwanzo ya Manzese -Sinza jijini Dar ambapo mara baada ya kesi kuahirishwa, alizungumza kilachotokea siku hiyo.

“Nimefika hapa mahakamani lakini mwenzangu ninayemshtaki hakufika hivyo kesi imeahirishwa hadi tarehe 12, mwezi wa nane. Kifupi nimeleta kesi ya madai na kesi ziko mbili, ya kwanza nilimetea mdhamini kaingiza hela natakiwa nilipwe.

“Ya pili ni kazi ya tangazo. Nimefanya tangazo kwa ajili ya Nandy Festival nikashangaa tangazo amelirusha hajanilipa ninamdai Nandy Milioni 25,” alisema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live