Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku afunguka chanzo cha ugomvi wake Harmonize, amtaja Paula

Mwijaku Harmo Paula Mwijaku afunguka chanzo cha ugomvi wake Harmonize, amtaja Paula

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji na chawa maarufu wa Konde Gang, Burton Mwemba ‘Mwijaku’ ameamua kuanika chanzo cha ugomvi wake na Harmomize baada ya taarifa kuanza kusambaa kuwa wawili hao kwa sasa wametofautiana.

Jambo hilo limesababisha Harmomize kum-block Mwijaku mpaka sasa huku chanzo kikitajwa kuwa ni ni Paula ambaye ni mtoto wa Kajala.

Akizungumza na moja ya vyombo vya habari nchini, amesema kuwa; “Harmonize nimemshauri vitu vya msingi laki ameniona mimi mpumbavu, anatembea na mama na mtoto, eti namshauri asirudie makosa eti anani-block.

“Amemfungulia Paula duka la milioni 20, unahisi hizo zimetoka bure tu. Yote haya nafanya kwa sababu nampenda Harmomize na sitaki apotee njia, nitahakikisha anaacha mambo yasiyofaa.

“Angekuwa anampenda Paula asingekuwa anampost uchi, siku akimpost Kajala na vile vinguo namshtaki, akimpost Paula nitamshtaki,” amesema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live