Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku: Nandy atalipa pesa yangu hata kama amekufa

Nandy Mwijaku Mwijaku na Nandy

Fri, 22 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa Clouds Media, Burton Mwenda ‘Mwijaku’ ameapa kuwa lazima msanii Faustina Mfinaga ‘Nandy’ amlipe pesa yake anayodai walikubaliana la sivyo atailipa hata kama amekufa.

Mwijaku amesema hayo leo Julai 22, 2022, kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM wakati akihojiwa kuhusu kutofautiana kwake na Nandy na kusababisha sauti za wawili hao wakitifuana kusambaa mitandaoni.

Tumsikie Nandy

“Sitaki kuongelea hilo suala, nitamvunjia heshima, nyie (Clouds FM) mnafanya naye kazi hapo kwa hiyo mnajua alichofanya kila kitu. Chanzo mbona hata yeye alikuwa anaongea, mbona watu wengi wanajua. Hamna jipya hapa duniani, limetokea amefanya litapita kwa sababu nishazoea hivi vitu.“

Tumsikie Mwijaku

“Kweli sauti inaotembea ni ya kwake Nandy, na nimwambie tu kwamba hela yangu atailipa, kama sio duniani basi hata mbinguni, nimetangulia ametangulia, yani mwili wake hauzikwi bila kulipa hela yangu. Na mimi sizikwi mpaka hela yangu niipate, yani nimeweka nadhiri leo ya umri jumaa.

“Nife mimi afe yeye, ridhiki yangu lazima niipate, na nitaandika katika urithi wangu mali Chui alipwe, nimeamua. Nandy anapenda hela, mimi nimefanya masoko miaka 10, nikifanya kazi nikaingiza hela nipe hela yangu.

“Tulikubaliana tena kikubwa Zaidi ya hichi baada ya kuona amepitia kwenye misukosuko ya harusi, nikasema lipa asilimia 10 ya malipo yote kama consultant niliyofanya, siwezi kutumia akili yangu, muda wangu, ku-edit proposal kupeleka halafu wewe upate.

“Anakaa anapiga picha na hela na mume wake wakati ni jasho langu, alete pesa zangu. Nimeshamwambia Billnass hana maamuzi kwa sababu dili sikufanya nay eye nilifanya na mkewe. Nimesema hakuna ndugu yangu atakayenizika kabla sijalipwa pesa zangu, na atakayetokea nitamkaba, na Jumamosi nakwenda Kigoma,” amesema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live