Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku: Kizz Daniel kufanya Buga Remox na Harmonize

Kizz Harmo.png Mwijaku: Kizz Daniel kufanya Buga Remox na Harmonize

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji huyo wa Clouds Media, Burton Mwenda 'Mwijaku' amethibitisha kuwa staa huyo wa muziki kutoka nchini Nigeria yupo nyumbani kwa Harmonize na huenda wakarekodi Buga Remix.

Mbali na hilo Mwijaku ameweka wazi kuwa Harmonize ndiye aliyempelekea nguo Kizz Daniel hoteli ila alizikataa na kusema hawezi kuvaa pia cheni alikataa na baadaye Harmonize kumletea designer na kuzikataa nguo zao.

Mbali na hilo Kizz Daniel alitaka GUCCI original nyeusi full na viatu vyeupe, alikataa mpaka cheni za Harmonize ameongeza Mwijaku akizungumza na @el_mando_tz

Ameongeza kuwa Kizz Daniel ametakiwa kulipa milioni 400 na zote Harmonize atamlipia hapa Tanzania maana yeye hawezi kulipa akiwa nje ya nchi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live