Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku: Diamond hajalipwa mil. 220 kwa dakika 10

Mwija Na Diamond Mwijaku: Diamond hajalipwa mil. 220 kwa dakika 10

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

DC wa Instagram, Mwijaku amefunguka kuwa, habari iliyozagaa kwenye mitandao na vyombo mbalimbali vya habari kuwa amefanya shoo nchini Kenya na kulipwa shilingi mil. 220 kwa dakika 10 si kweli.

Mwijaku alisema, habari hiyo ni ya uongo na inaleta chuki kwa wasanii wa Kenya kuona kama staa huyo alilipwa zaidi ya wenzake wakati wasanii walilipwa sawasawa.

“Ni uongo tu kwanza mnatengeneza chuki kwa wasanii wa Kenya. Nimefatilia, Mwijaku hapana ni uongo. Wasanii wote walipafomu pale walipewa dakika 10, walilipwa milioni 45. Yeye alilipwa milioni 40, kilichozidi ni kimoja alisema mimi natokea Sauz ndio akaongezewa gharama za usafiri.

“Hata hivyo alipewa private jet ya Raila Odinga hivyo utaona watu tu wamejiongeza kwa kusema amelipwa milioni 220,” alisema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live