Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku : Diamond alinifanya nijenge

Mwijaku: Diamond Anapoongeza Msanii, Na Sisi Tunapata Riziki Mwijaku : Diamond alinifanya nijenge

Sun, 7 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Dc wa Instagram @mwijaku Ameandika....

"#UKWELI-Siwezi kupinga ukweli ..! Safari yangu ya kwanza QATAR ( WorldCup ) na malipo yake ndio yalio nifanya ninunue eneo na kuanza safari yangu ya kujenga KASRI langu ( Ndoto yangu )

Ukweli usemwe , Ulinipa rizki kupitia kampuni yako, nami nikaitumia vizuri , sitakii kuwa mchoyo ya kushukuru, nakumbuka tulipokuwa Qatar ulinambia kuwa; "pambana wakati wako huu DC " nami nikaichukua hiyo kauli .

Tarehe 5/01/2024 Nimekamilisha ndoto yangu . Kupitia Kampuni yako ilinipa mkataba zaidi ya miaka miwili na malipo ya kila mwezi na nikatumia kama sehemu ya uwekezaji kwangu .

Nasema Asante MWAMBINO. @diamondplatnumz sitaki kuja kusubiria ukifa au nikifa ndio yasemwe haya . Ulinifaa wakati wa shida na wakati wa mahitaji Muhimu .

Asante kwa @donfumbwe Nakumbuka mzigo ulio nipa magomeni usiku wa saa mbili baada ya kupokea simu toka kwa mwambino ndio ulizaa uwekezaji huuuu . Asante kwako kwa kua hukunizunguusha kunikabidhi haki yangu.

Nimshukuru pia mama mzazi wa MWAMBINO @mama_dangote , ulinipa ushirikiano mkubwa pale QATAR na kunambia fanya kazi uisaidie familia yako na niache CHUKI binafsii . Nika kwambia simchukii MWAMBINO but ni kuchangamsha mitandao yetu . Asante kwa kunielewa mama yangu .

Haya Mengine ya mtandaoni ni sehemu zetu za kunogesha game na kuhakikisha tunapambana kukuza burudani .

Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa fikra za kuwasaidia wengine kwa kuwapa kazi na kuwapa usia wa kutumia vizuri vipato wanavyo vipata . Asante kwa hili MWAMBINOOO

Mungu akubariki wewe na kizazi chako . Sema na mimi nakushaurii OA mkubwa wakati wako huu Muoe ZUCHU @officialzuchu ana UPEPOO WAKO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live