Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku: Diamond ajirekebishe

Diamond Urenoooo Diamond Platnumz

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa Clouds Media, Burton Mwenda 'Mwijaku' ameiponda shoo ya supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aliyoifanya hivi karibuni nchini Ureno akimtaka msanii huyo ajirekebishe na kuboresha namna ya kutumbuiza jukwaani na si kuruka sarakasi na kuwamwagia maji mashabiki.

Akizungumzia shoo hiyo ya ya AFRONATION, Mwijaku ameilinganisha na shoo ya supastaa wa Nigeria, Burna Boy akisema Diamond amezidiwa vitu vingi na staa huyo.

Mwijaku ameenda mbali akisema kama ili wasanii wa Tanzania waweze kufanikiwa, basi ni lazima waambiwe ukweli ili wajirekebishe.

“Huwezi kuwa best performer kwa kuwapigia watu kelele na kuruka sarakasi, imba watu wanahitaji uimbe."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live