Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijaku Atajwa Chawa Ghali Zaidi

Mwijaku Mondi Mwijaku Atajwa Chawa Ghali Zaidi

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Enzi hizo, sanaa na burudani ilikuwa siyo rasmi. Watu walicheza michezo na kufanya sanaa kwa mapenzi yao tu; wala siyo kwa ajili ya pesa.

Lakini maisha yanabadilika, hivi sasa burudani na sanaa kwa jumla imekuwa sekta rasmi kabisa na watu kibao wanaingiza mkwanja mrefu.

Hivi sasa, Kanye West, Elton John, Ariana Grande, Jonas Brothers, Chainsmokers, Ed Sheeran, Taylor Swift na Post Malone ni baadhi ya wanamuziki wanaoingiza mkwanja mrefu sana kupitia sanaa ya muziki.

Stephen Curry, James Harden, John Wall, Russell Westbrook, Damian Lillard, LeBron James na Kevin Durant ni baadhi ya wachezaji wa basketball wanaoingiza mkwanja mrefu kupitia mchezo wa basketball.

Ronaldo, Messi, Neymar, Kylian Mbappe na Mohamed Salah ni baadhi ya footballers wanaoingiza mkwanja mrefu kupitia mchezo huo.

Kibongobongo Mwijaku ni chawa ambaye anaingiza mkwanja mrefu kupitia uchawa wake. Uchawa wake ni very professional wa kisomi zaidi.

Ili Mwijaku awe chawa wako inabidi umlipe pesa nyingi, siyo kama wale chawa wa upande wa pili wanaonunuliwa kwa bei rahisi.

Mwijaku ameheshimisha tasnia ya uchawa, hivi sasa kila kijana anatamani kuwa chawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live