Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigizaji wa Kenya afariki Dunia

Charlie Mwigizaji wa Kenya afariki Dunia

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji maarufu wa Kenya Charles Ouda almaarufu kama Charlie amefariki dunia.

Familia ya Muigizaji huyo imethibitisha kutokea kwa msiba huo Jumamosi usiku, hata hivyo sababu za kifo chake hazijatajwa.

Familia imeomba watu wote kuheshimu faragha ya mchumba wa marehemu, Bi.Ciru Muriuki pamoja na familia nzima.

Bi.Muriuki ,mtangazaji wa zamani wa BBC Africa pamoja na marehemu walitangaza kuvishana pete ya uchumba Septemba mwaka jana.

Ouda hakuwa tu muigizaji, bali pia muandaaji na muongozaji wa filamu, Mwandishi wa nyimbo, Msanii wa sauti, Meneja wa matukio na mtangazaji wa televisheni.

Mtaalamu huyo wa sanaa anajulikana zaidi kwa kipindi maarufu cha watoto ”Know Zone” na tamthilia ya ”Makutano Junction”.

Wakati wa uhai wake, Ouda alijipatia tuzo mbalimbali ikiwemo ya muongozaji bora kwa mwaka 2016.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live