Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigizaji wa Filamu Marekani afariki Dunia

Johnny Wactor 052624 1 5740b94ba2b1485ab4f00f1964fc8dc6 Mwigizaji kutoka Marekani Johnny Wactor

Mon, 27 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji kutoka Marekani Johnny Wactor ambaye alijulikana zaidi kupitia tamthilia ya ‘General Hospital’ amefariki dunia kwa kupigwa risasi katika moja ya mtaa wa Los Angeles.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na mama yake mzazi Scarlett Wactor ambapo aliviambia vyombo vya habari siku ya jana Jumapili Mei, 26, 2024 kuwa mwanaye alipigwa risasi na wezi watatu waliotaka kuiba kwenye gari lake siku ya Jumamosi asubuhi.

Wactor amefariki akiwa na umri wa miaka 37, huku akionekana kwenye tamthilia kama ‘#Lifetime’, ‘Hollywood Girl’, ‘The Passenger’ na nyinginezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live