Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigizaji wa Black Panther afariki na watoto wake watatu

Taraj Ramsesss Mwigizaji wa Black Panther afariki na watoto wake watatu

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani, TarajaRamsess amefariki dunia akiwa na watoto wake watatu baada ya gari lake kugonga trekta.

Taraja ambaye ameonekana katika movie ya Black Panther alifariki baada ya gari lao kugonga trekta lililokuwa limeharibika katikati ya barabara katika kaunti ya Dekalb, Georgia usiku ambapo alikuwa na watoto wake 5.

Taarifa hiyo, imetolewa rasmi na familia ya muigizaji huyo kwa kueleza kuwa watoto hao watatu ambao ni Sundari (13), Fuginop (10) na mwingine wa wiki nane wote wamefariki na baba yao katika ajali hiyo huku watoto wawili wakiwa hospitali wakiendelea kupatiwa matibabu.

Ikumbukwe kuwa mwamba huyo alionekana katika filamu mbalimbali ikiwemo Black Panther, Avengers, Avengers: Infinity War na nyinginezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live