Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigizaji arudisha kitabu alichochukuwa maktaba miaka 47 baadaye

Collage (12) Mwigizaji arudisha kitabu alichochukuwa maktaba miaka 47 baadaye

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Ilikuwa ni afadhali kuchelewa kuliko kutorejesha kabisa kitabu alichokipata mwigizaji Uri Geller.

Aligundua hivi majuzi kitabu cha takriban miongo mitano wakati akipekua masanduku katika chumba chake cha kuhifadhia vitu huko Israel.

Alipata kitabu - kuhusu yeye mwenyewe - ambacho alikuwa amechukua kutoka kwa Maktaba ya Umma ya Los Angeles miaka 47 iliyopita.

Bw Geller aliazima kitabu hicho mnamo Januari 1977.

"Ninafungua sanduku na kuanza kutoa vitabu na mbele yangu nikakutana na karatasi ya manjano," aliambia BBC News.

Mwanaume huyo ambaye sasa yuko katika miaka yake ya 70, alisema kwamba aliondoka Israel mwaka 1972 na kuelekea Marekani kushiriki katika majaribio kadhaa yaliyofanywa na CIA kuchunguza uwezo wake wa kiakili.

Kundi la wanasayansi lilimchunguza sana Bw Geller, na kusababisha kuchapishwa kwa jalada lake ‘The Geller Papers’ mnamo mwaka 1976.

Ilijumuisha mkusanyiko wa karatasi za kisayansi zinazoeleza kwa kina uchunguzi na majaribio aliyofanyiwa alipokuwa Marekani.

Kitabu cha Bw Geller, kilinunuliwa sana.

Aliishia kurejea nacho New York lakini "akakisahau kabisa" kukipeleka maktaba.

Alikipata alipokuwa akipekua-pekua masanduku ya kuhifadhia.

Bw Geller aliyejiita mhifadhi, alisema "alifurahi" mno alipokipata kitabu hicho.

"Nilipokiona, jambo la kwanza lililonijia ni: 'Wow, nimepitia mengi sana maishani mwangu," alisema.

Chanzo: Bbc